Uruk
, king of Uruk Uruk (jina katika Biblia: Erech; jina la leo kwa Kiarabu: وركاء warkā) ilikuwa mji wa Wasumeri katika Mesopotamia ya Kale. Baadaye ilikuwa sehemu ya milki ya Babeli. Mahali pake palikuwa kando la mto Frati uliohama na kupita sasa 30 km kutoka mahali pa Uruk.
Uruk ilikuwa mahali muhimu katika maendeleo ya miji katika Mesopotamia wakati wa milenia ya 4 KK. Kipindi chake cha kustawi hasa kilikuwa mnamo mwaka 2900 KK ilipokuwa na wakazi 50,000 – 80,000 waliokalia eneo la kilimita za mraba 6 ndani ya kut zake.
Mfalme mashuhuri wa mji huu alikuwa Gilgamesh manmo mwaka 2600 KK. Wakati wa vita kati ya Babeli na Elami umuhimu wa Uruk uliungua. Watu waliendelea kuishi hapa kwa karne nyingi hadi wakati wa nasaba ya Sassanidi miaka michache kabl ya upanuzi wa Uislamu.
Mahali pa Uruk palitambuliwa tena 1849 na wanaakiolojia chini ya William Kennett Loftus aliyeongoza uchimbaji hapa kuanzia 1850.
Inaaminiwa ya kwamba jina la Kiarabu "Iraq" kwa sehemu ya kusini ya Mesopotamia limetokana na Uruk.
Viungo vya Nje
hariri- Earliest evidence for large scale organized warfare in the Mesopotamian world (Hamoukar vs. Uruk?
- Uruk at CDLI wiki
- Lament for Unug Archived 5 Juni 2011 at the Wayback Machine. (sux)
- Archaeological Expedition Mapping Ancient City Of Uruk in 2002
- Digital images of tablets from Uruk - CDLI Archived 17 Juni 2011 at the Wayback Machine.