Usafi wa mazingira ulioboreshwa

Usafi wa mazingira bora ni neno ambalo linatumiwa kutofautisha aina au ngazi ya Usafi wa mazingira kwa lengo la ufuatiliaji. Neno hili liliundwa na Mpango wa ufuatiliaji wa pamoja (JMP) kwa usambazaji wa maji na Usafi wa mazingira wa UNICEF na WHO katika mwaka wa elfu mbili na mbili ili kusaidia kufuata maendeleo kuelekea lengo la saba la Malengo ya maendeleo ya milenia (MDG). Neno kinyume la “usafi wa mazingira ulioboreshwa” ni “usafi wa mazingira ambayo hajaboreshwa” katika ufafanuzi wa JMP.

Mpango wa ufuatiliaji wa pamoja (JMP) kwa usambazaji wa maji na Usafi wa mazingira huchapisha habari za hali ya usafi wa mazingira duniani kila mwaka. Kwa mfano, katika mwaka wa elfu mbili na kumi na tano iliripotiwa kwamba asilimia sitini na nane ya idadi ya watu duniani ilikuwa na upatikanaji wa usafi wa mazingira ulioboreshwa.[1]

Katika mwaka wa elfu mbili na kumi na saba, JMP iliunda neno jipya: “huduma ya msingi ya usafi”. Neno hili linatajwa kama matumizi ya vifaa vya usafi ambavyo wa bora ambavyo hazikushirikiwa na kaya nyingine.

Kiwango cha chini cha huduma sasa inaitwa “huduma ya usafi ya ndogo” ambayo inahusu matumizi ya vifaa vya usafi ambavyo vimeboreshwa ambavyo ni vinatumia kati ya kaya mbili au zaidi.

Kiwango cha juu cha huduma inaitwa “usafi wa mazingira unaosimamiwa salama”. Hii ni aina ya huduma ya usafi wa msingi inahitajika kuwa salama katika situ au zinasafirishwa na kuchukuliwa mahali pengine.[2]

Ufafanuzi hariri

Mdogo, msingi, na kusimamiwa salama usati wa mazingira hariri

Katika mwaka wa elfu mbili na kumi na sita, JMP iliunda maneno matatu mapya:[2]

  • “Huduma ya msingi wa usafi”. Hili linatajwa kama matumizi ya vifaa vya usafi ambavyo vimeboreshwa ambavyo hazikushirikiwa na nyumba nyingine.
  • Kiwango cha chini cha huduma kuliko huduma ya usafi wa msingi sasa inaitwa "huduma ya usafi ya ndogo" ambayo inahusu matumizi ya vifaa vya usafi ambavyo vimeboreshwa ambavyo vinatumia kati ya kaya mbili au zaidi.
  • Kiwango cha juu cha huduma kuliko huduma ya usafi wa msingi unaitwa “usafi wa mazingira unaosimamiwa salama”. Hii ni aina ya huduma ya usafi ya msingi ambayo hutuma taka kwa situ au mahali pengine.

Usafi wa mazingira bora hariri

 
Mfano wa usafi wa mazingira: Choo cha shimo na slab inayofunika shimo la kushuka na kituo cha kuosha mikono nchini Burundi.

Kifaa cha usafi ni kifaa kimoja ambacho kinaweza kuchotenganisha taka ya binadamu kutoka kugusa na binadamu. [3] Kifaa hiki si sawa na usafi wa mazingira endelevu.

Kuruhusu kulinganisha duniani kote ya makadirio ya ufuatiliaji Malengo ya maendeleo ya milenia (MDG), Mpango wa ufuatiliaji wa pamoja (JMP) kwa usambazaji wa maji na Usafi wa mazingira inafafanua "usafi wa mazingira ulioboreshwa" kama aina za vyoo zifuatazo:

  • Choo cha kusafisha
  • Choo cha kuungana na mfumo wa septic
  • Flush / kumwaga maji-flush katika choo cha shimo
  • Choo cha shimo na slab
  • Choo cha shimo na ufunguzi wa hewa
  • Choo cha mbolea

Usafi wa mazingira ambayo hayajaboreshwa hariri

 
Mfano usiohifadhiwa wa usafi wa maji: Choo cha shimo bila slabi huko Lusaka, Zambia.

Vifaa vya usafi wa mazingira ambayo siyo “kuboreshwa” (unaitwa "hayajaboreshwa" pia) ni:

  • Choo cha umma au cha pamoja (maana ya choo ambacho ni hutumia kati ya zaidi ya moja ya kaya).
  • Flush / kumwaga maji-flush katika mahali pengine (sio ndani maji taka, shimo, au tank ya septic).
  • Choo cha shimo bila slab
  • Choo cha ndoo
  • Choo kilichoinuliwa
  • Hakuna vifaa / kichaka / shamba [4]

Marejeo hariri

  1. Progress on sanitation and drinking-water : 2014 update. World Health Organization., UNICEF. Geneva. ISBN 9789240692817. OCLC 889699199. 
  2. 2.0 2.1 Progress on drinking water, sanitation and hygiene : 2017 update and SDG baselines. World Health Organization,, UNICEF,. Geneva. ISBN 924151289X. OCLC 1010983346. 
  3. "Figure 13.19. Access to improved water sources and sanitation facilities (2000 and 2015)". dx.doi.org. Iliwekwa mnamo 2019-04-15. 
  4. WHO/UNICEF Joint Water Supply and Sanitation Monitoring Programme. World Health Organization, issuing body. UNICEF, issuing body. Progress on drinking water and sanitation. ISBN 9789241507240. OCLC 890621984.