Utalii wa Botswana

Vivutio vikuu vya watalii vya Botswana ni mapori ya akiba, pamoja na uwindaji na safari za kupiga picha. Vivutio vingine ni pamoja na eneo la Delta ya Okavango [1], ambalo wakati wa mvua maji upita, visiwa na maziwa. [2] Sekta ya utalii pia ilisaidia kuleta ukuaji wa uchumi wa Botswana kutoka vyanzo vya jadi kama vile almasi na nyama ya ng'ombe na kutoa nafasi za kazi 23,000 mwaka wa 2005. [3]

Takwimu hariri

Mwaka wa 1999, kulikuwa na vyumba 2,100 vya hoteli na vitanda 3,720 na kiwango cha 53% cha watu wanaokaa. Wageni 843,314 waliwasili Botswana mwaka huo na zaidi ya 720,000 kutoka nchi nyingine za Afrika. Mapato ya utalii katika mwaka wa 2000 yalifikia dola milioni 313. Mwaka 2003, Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilikadiria wastani wa gharama ya kila siku ya kukaa Gaborone kuwa $129, ikilinganishwa na Kasane ya $125. Gharama iliweza kushuka chini hadi $50 katika maeneo mengine ya nchi. [4] Botswana inachukuliwa kuwa nchi salama zaidi kutembelea barani Afrika. [5]

Wageni wengi waliofika Botswana wakati wa likizo zao walitoka nchi zifuatazo : [6]

Nchi 2016 2015 2014 2013
  Zimbabwe 874,169 967,322 784,720 825,717
  South Africa 759,564 808,118 600,387 742,639
  Zambia 220,649 202,289 188,351 331,799
  Namibia 187,044 170,326 162,453 169,733
  United States 52,171 49,451 49,961 139,752
  United Kingdom 42,534 41,011 39,675 47,929
  Germany 35,288 32,230 34,576 43,674
  India 19,297 17,413 18,342 13,543
  Lesotho 18,773 18,842 12,408 10,839
  Malawi 17,102 20,607 15,175 17,386
Total 2,401,786 2,501,616 2,082,521 2,598,158

Marejeo hariri

  1. Ross, Karen (1987). Okavango, jewel of the Kalahari. London: BBC Books. ISBN 0-563-20545-8. OCLC 17978845. 
  2. Nations Encyclopedia
  3. Kajevu, Zeph. "Ranking worries BNPC", allAfrica.com, 2008-04-08. 
  4. Nations Encyclopedia
  5. Travel Risk Index: Botswana. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-02-18. Iliwekwa mnamo 2012-08-10.
  6. Tourism Statistics Annual Report 2014