Utenzi wa inkishafi

Utenzi wa inkishafi ni moja kati ya tungo za kale sana ambazo zimeweza kuhifadhiwa na kuonekana hadi leo. Ni tungo ambayo imejadiliwa katika makongamano mengi ya Kiswahili kutokana na mtindo na maudhui yaliyotumika katika utenzi huu.

Kuna madai ambayo hayajathibitishwa kuwa kikamilifu kuwa inkishafi ulitokana na tungo za Kiswahili za zamani ziitwazo shairi la Qala al Muhadhar [1]

Utenzi huu ulitungwa mwaka 1853 na nakala hii iliweza kupatikana katika milki ya Sayyed Munsab ambaye alihusiana kinasaba na mtunzi wa utenzi huu, Sayyed Abdallah Bin Ally. Watafiti wengi wa lugha ya Kiswahili wamekuwa wakitumia utenzi huo katika kuchunguza mambo mbalimbali yanayohusu lugha na fasihi ya Kiswahili.

Tanbihi

hariri
  1. Tenzi tatu za kale. Mulokozi, M. M. (Mugyabuso M.), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es Salaaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. 1999. ISBN 9976-911-34-3. OCLC 45248518.{{cite book}}: CS1 maint: others (link)
  Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utenzi wa inkishafi kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.