Nasaba ikitumiwa kwenye masomo ya historia au siasa inataja ufuatano wa watawala hasa wafalme katika familia moja. Mtoto wa mfalme huwa mfalme tena na kadhalika.

Neno laweza kutaja pia kipindi cha historia ambako familia fulani ilitawala.

Kati ya nasaba za kifalme za leo ni hasa nasaba ya Matenno wa Japani iliyodumu muda mrefu. Tangu Tenno wa kwanza ni watawala 125 wanaohesabiwa katika familia hiyohiyo hadi Kaisari au Tenno Akihito wa leo.

Nasaba nyingine inyojulikana duniani ni Windsor na malkia Elizabeth II wa Uingereza ni wa nne katika nasaba hii nchini Uingereza.

Katika Afrika familia ya wafalme wa Eswatini iko kati ya nasaba za kale zinazoendelea kutawala. Nasaba ya Suleimani iliyotawala Ethiopia tangu 1270 BK ilipinduliwa katika mapinduzi ya 1974.

Historia ya Misri ya Kale hupangwa kufuatana na nasaba 33 za mafarao wake hadi malkia Kleopatra.