Uwanja wa michezo wa Dobsonville
Uwanja wa michezo wa Dobsonville (zamani ulijulikana kama uwanja wa michezo wa Volkswagen Dobsonville, pia ulitambulika kama uwanja wa Dobsie) ni uwanja wa michezo wenye matumizi mengi huko Soweto, kiunga cha jiji la Johannesburg, Afrika Kusini. Uwanja upo chini ya usimamizi wa viwanja SMSA.
Mara nyingi uwanja huu unatumika kwa michezo ya shirikisho la mpira wa miguu na pia ina sehemu ya michezo ya riadha. Ni uwanja wa nyumbani kwa klabu ya Moroka Swallows F.C, klabu iliyocheza ligi kuu mpaka iliposhuka daraja mwishoni mwa msimu wa mwaka 2014-15.[1] Pia ilitumika kama uwanja wa mazoezi kwa timu zilizoshiriki kombe la dunia ya mnamo mwaka 2010 baada ya maboresho yaliyofanyika na kufikia viwango vya FIFA.
Uwanja wa Dobsonville ulijengwa mnamo mwaka 1975 na ulikuwa na uwezo wa kubeba washabiki wapatao 20,000 na kwa sasa ina uwezo wa kubeba washabiki wapatao 24,000 pakiwa na maboresho katika eneo la waandishi wa habari, vyumba vya kubadili mavazi, vyumba vya mazoezi ya mwili na maeneo ya kufanyia mikutano.
Uwanja wa Dobsonville ulianzishwa kama uwanja wa michezo mwaka 1957 kipindi ambapo watu wa magharibi ya Roodepoort waliporejea kwenye makazi yao. Palikuwepo viwanja vingi vya mpira wa miguu ila uwanja huu ndio uliokuwa unajulikana sana.
Matukio mengi ya kimataifa yaliwahi kufanyika katika uwanja wa Dobsie kama vile mashindano ya mpira wa miguu kwaa vijana walio na umri chini ya miaka 20 ya mwaka 2009, mashindano ya Gauteng ya mwaka 2010 na pia baadhi ya michezo ya kitaifa ya mpira wa miguu ya Afrika Kusini kama vile mchezo wa Banyana Banyana (timu ya taifa ya wanawake ya Afrika Kusini).
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-03. Iliwekwa mnamo 2021-06-08.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Dobsonville kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |