Uwanja wa michezo wa Orlando
Uwanja wa michezo wa Orlando ni uwanja unaotumika kwa michezo mbalimbali huko Soweto kitongoji cha Johannesburg kilichopo Gauteng nchini Afrika Kusini. Ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya mpira wa miguu ijulikanayo kwa jina la {Orlando Pirates}, timu mashuhuri ya soka ambayo hucheza katika Ligi kuu ya soka ya {Afrika Kusini}.[1] [2] [3]
Historia
haririUwanja huu hapo awali ulijengwa na Chama cha soka cha {Johannesburg Bantu} ambapo ulikuwa na uwezo wa kukaa watu wapatao elfu ishirini na nne (24,000) ambapo matengenezo yaligharimu kiasi cha £37,500. Ulifunguliwa na Waziri wa maendeleo ya Bantu, MC de Wet Nel na (Ian Maltz) ambaye kwa wakati huo alikuwa Meya wa Johannesburg mnamo tarehe 2 Mei 1959.[4][5]
Mnamo mwaka 1978, timu ya Soka ya Orlando ilimchukua (Phil Venter) ambaye alikuwa mchezaji mweupe wa kwanza wa Shirikisho la soka Kitaifa kuichezea timu ya watu weusi. Badae alijiunga na mchezaji mwingine mweupe aitwaye (Keith Broad).[6]
Mnamo mwaka 1995, Uwanja huo ulikuwa mwenyeji katika mazishi ya Kigogo wa African National Congress ajulikanaye kama Joe Slovo, na pia yale ya Walter Sisulu yaliyotokea mnamo mwaka 2003 ambapo Thabo Mbeki, Nelson Mandella, Joaquim Chissano wa Mozambique, Robert Mugabe wa Zimbabwe, na Pakalitha Mosisili wa Lesotho alikuwa miongoni mwa waombolezaji walioshiriki.[7] [8]
Mnamo mwaka 2011, uwanja huo pia uliandaa mazishi ya Albertina Sisulu ambapo Jacob Zuma, Jakaya Kikwete wa Tanzania na Kenneth Kaunda wa Zambia walikuwa miongoni mwa waombolezaji, pia katika mazishi ya Winnie Mandela mnamo mwaka 2018 ambapo Cyril Ramaphosa, Raisi wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, Kgalema Motlanthe, Jacob Zuma, Hage Geingob wa Namibia, Denis Sassou Nguesso wa Kongo-Brazaville na Mokgweetsi Masisi wa Botswana na Naomi Campbell wa (Britain) walikuwa kati ya waombolezaji walioshiriki.
Viungo vya nje
hariri- Stadium history
- Stadium Management South Africa Archived 18 Oktoba 2021 at the Wayback Machine.
Marejeo
hariri{
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Orlando kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-06-15. Iliwekwa mnamo 2021-06-12.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-12. Iliwekwa mnamo 2021-06-12.
- ↑ https://www.travelground.com/attractions/orlando-stadium
- ↑ "History of Orlando Stadium". Soweto Urban. 7 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 14 Aprili 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Moya, Fikile-Ntsikelelo (15 Desemba 2005). "A fitting farewell to Orlando Stadium". The M&G Online (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 14 Aprili 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Defending Football". The Witness. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Oktoba 2014. Iliwekwa mnamo 17 Juni 2013.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ [1], Orlando Stadium History, Joburg.org.za, accessed 6 June 2013
- ↑ https://sowetourban.co.za/17872/history-of-orlando-stadium/