Uwanja wa michezo wa Saxon-Sea
Umetengenezwa huko Afrika Kusini
Uwanja wa michezo wa Saxon-Sea ni uwanja wa michezo unaotumika kwa michezo mbalimbali katika maeneo ya Saxonsea wilaya ya Atlantis, mji ulio kilometa arobaini (40) kaskazini mwa mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini. Mara nyingi umekuwa ukitumika kwa mechi za mpira wa miguu. Mnamo mwaka 2010 ulitumika kama ukumbi wa nyumbani wa timu ya mpira wa miguu ya Jomo Powers F.C., ikicheza mkoa wa Western Cape katika mchezo wa Ligi ya Vodacom.