Rasi ya Magharibi

(Elekezwa kutoka Western Cape)
Rasi ya Magharibi
Western Cape
Wes-Kaap
Ntshona-Koloni
(Nembo la Jimbo la Rasi Magharibi)
Mahali pa jimbo la Rasi Magharibi
Mji Mkuu Cape Town
Mji Mkubwa Cape Town
Waziri Mkuu Helen Zille
Eneo
- Jumla
Nafasi ya 4 kati ya majimbo ya Afrika Kusini
129,370 km²
Wakazi
 - Total (2001)
 - Msongamano wa watu
Nafasi ya 5 kati ya majimbo ya Afrika Kusini
4,524,335
35/km²
Milima Sehemu ya juu: Seweweekspoort Peak yenye 2,325 m
Sehemu ya duni: Uwiano wa bahari
Lugha Kiafrikaans (55.3%)
Kixhosa (23.7%)
Kiingereza (19.3%)
Wakazi kimbari Chotara (53.9%)
Waafrika Weusi (26.7%)
Wazungu (18.4%)
Waasia (1.0%)


Rasi ya Magharibi ni moja kati ya majimbo 9 ya Afrika Kusini. Mji Mkuu ni Cape Town (Kaapstad). Jimbo liliundwa mwaka 1994 kutokana na maeneo ya Jimbo la Rasi la awali.

Demografia na utamaduni

hariri
 
Groot Constantia - nyumba ya kihistoria ya Waholanzi mamabu wa makaburu

Idadi ya wakazi ilikuwa 4,524,335 mwaka 2004. Zaidi ya nusu ya wakazi hutumia Kiafrikaans kama lugha ya kwanza (55,3%), takriban robo Kixhosa (23,7%) na karibu sehemu ya tano Kiingereza (19,3%). Lugha hizi tatu ni pia lugha rasmi za jimbo.

Eneo la jimbo lilikuwa chanzo cha Afrika Kusini ya kisasa. Historia imeonekana pia kati ya wakazi. Idadi kubwa ni watu wenye uzazi wa chotara hasa wa Waafrika, Wazungu na Waasia waliopelekwa hapa kama watumwa katika karne ya 18. Kati ya Waafrika Weusi kundi kubwa ni Waxhosa. Wazungu ni wa asili ya Kimakaburu na Kiingereza hasa. Rasi Maghribi ina pia jumuiya kubwa ya Waislamu iliyoanzishwa na watumwa Waasia kutoka Asia Kusini-Magharibi.

Jiografia

hariri
 
Rasi ya Afrika Kusini

Rasi Magharibi ni sehemu ya kusini kabisa ya bara la Afrika. Ncha yake ni rasi Agulhas yenye umbali wa 3,800 km na ncha ya kusini. Eneo lake ni 129,370 km² au 10% za Afrika Kusini yote.

Rasi Magharibi imepakana na majimbo ya Rasi Kaskazini na Rasi Mashariki. Kuna pwani ndefu za Atlantiki na Bahari Hindi. Visiwa vya Prince Edward katika bahari ya Hindi ya Kusini zinatawaliwa na jimbo.

 
Bonde lenye rutba katika Rasi magharibi

Mito mikubwa ni Breede na Berg.

Miji mikubwa pamoja na mji mkuu wa Cape Town ni Stellenbosch, Worcester, Paarl na George.

 
Theluji katika wilaya ya Kouebokkeveld karibu na Ceres

Hali ya hewa hiathiriwa na maji baridi ya Atlantiki na maji ya vuguvugu ya Bahari Hindi. Kwa jumla hali ya hewa hufanana na Mediteranea. Hakuna joto kali lakini wakati wa baridi theluji hutokea mlimani. Uso wa nchi katika jimbo una sehemu nyingi sana. Eneo kubwa ni la milima inayofikia kimo cha 2300 m. Mabonde kati ya milima yana rutba.

Barani mbali na pwani na mvua zake kuna beseni ya Karoo ambayo ni kavu sana.

  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rasi ya Magharibi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.