Víctor Manuel Fernández

Víctor Manuel "Tucho" Fernández (alizaliwa 18 Julai 1962) ni kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Argentina na pia mtaalamu wa theolojia. Hivi sasa, ni mkuu wa Dikasteri ya Mafundisho ya Imani.

Víctor Manuel Fernández

Fernández aliwahi kuwa mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki cha Kipapa cha Argentina kuanzia Desemba 2009 hadi Aprili 2018. Mnamo tarehe 2 Juni 2018, aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa La Plata.

Tarehe 1 Julai 2023, Papa Fransisko alimteua Fernández kuwa msimamizi wa Dikasteri ya Mafundisho ya Imani kuanzia katikati ya Septemba mwaka huo. Aidha, tarehe 30 Septemba 2023, Papa Fransisko alimfanya Fernández kuwa kardinali.[1]

Marejeo

hariri
  1. Beltramo Álvarez, Andrés. "Argentina: Víctor Fernández es nuevo arzobispo de La Plata", La Stampa, 2 June 2018. (es) 
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.