Vampiri ni madubwana katika hadithi na hekaya. Hadithi za kwanza za vampiri zilihadithiwa huko Ulaya Mashariki, lakini watu wengi wanadhani vampiri waliundwa na Bram Stoker katika riwaya maarufu, Dracula. Watu wachache wanaamini kuwa vampiri wanaishi, lakini bado ni maarufu sana katika sinema, televisheni, na vitabu.

Vampiri
Vampiri.

Vampiri hapo zamani walikuwa watu lakini wana laana ya kiuchawi. Vampiri lazima wanywe damu ili kuishi. Wao hufanya hivyo kwa kuuma watu au wanyama kwenye shingo na meno yao mawili marefu. Watu ambao wanauliwa na vampiri kwa kunyonywa damu wanaweza pia kuwa vampiri kama wao baada ya kufa. Katika hadithi nyingi, vampiri wanaweza kubadilika kuwa wanyama wengine, kwa kawaida popo, ingawa pia mbwa mwitu, paka au panya.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vampiri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Lakin pia vampire wanaenezwa na virus wanaoitwa VBT-16