Popo
Popo-masikio wa Townsend (Corynorhinus townsendii)
Popo-masikio wa Townsend
(Corynorhinus townsendii)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Ngeli ya chini: Eutheria
Oda: Chiroptera (Wanyama kama popo)
Ngazi za chini

Nusuoda 2:
Megachiroptera (Popo-matunda) Microchiroptera (Popo-wadudu)

Popo ni mamalia kama panya mwenye mabawa.

Spishi zake nyingi sana hula wadudu: hizi zimo katika nusuoda Microchiroptera.

Spishi kubwa za nusuoda hii hula ndege, mijusi, vyura na hata samaki.

Spishi chache za popo mnyonya damu huko Amerika ya Kusini hula damu ya mamalia au ndege.

Nusuoda Megachiroptera ina spishi kubwa hadi ukubwa wa paka na uzito wa kilogramu moja; urefu wa mabawa pamoja unaweza kufikia sentimita 150. Spishi hizi hula matunda.

Popo wengi hutumia sauti kwa kutambua mazingira yao, yaani wanatumia mwangwi wa mlio wao kukadiria umbali hadi kizuizi au hata windo pamoja na ukubwa na maumbile ya vitu vilivyopo njiani. Kwa hiyo masikio yao ni mlango wa fahamu muhimu zaidi. Kinyume chake popo wengi hawana macho mazima ingawa hakuna aliye kipofu kabisa. Lakini kuna pia aina nyingine wanaoona vizuri sana.

Picha

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Popo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.