Victory
Victory ni filamu ya kimichezo ya 2009 ya India ambayo inaangazia mchezo wa Criketi, ambayo nyota wake ni Harman Baweja, Amrita Rao na Anupam Kher. Ni toleo la pili la Harman Baweja baada ya toleo lake la kwanza la Love Story 2050, ambayo haikutia fora katika Box Office. Movie hii ilinaswa nchhini Australia na India na inasemekana kuwa moja ya filamu zilizoigharimu Bolywood sana hadi leo.[1].
Victory | |
---|---|
Imetungwa na | AjitPal Mangat |
Nyota | Harman Baweja Amrita Rao Anupam Kher Gulshan Grover Several International Cricketers[1] |
Muziki na | Anu Malik |
Imetolewa tar. | 16 Januari 2009 |
Ina muda wa dk. | Dakika 159 |
Nchi | India |
Lugha | Hindi |
Filamu hii inamwangazia mwanacriketi mmoja ambaye anajitahidi kufanikiwa ambaye anapuuza vikwazo vyote ili kuifikia ndoto yake ambayo takribani haiwezekani.
Ploti
haririHadithi inaangazia maisha ya Vijay Shekhawat (Harman Baweja) na baba yake Ram Shekhawat (Anupam Kher). Ram ana maono makubwa kwa mwanawe Vijay ambaye anatarajia ataichezea timu ya taifa ya Criketi ya India. Ndoto yake hatimaye inatimia wakati Vijay anafuzu kwa timu hiyo. Rafikiye wa utotoni Nandini (Amrita Rao) ameuamini uwezo wake tangu mara ya kwanza alipotaja jina criketi na hakuwahi kumshuku. Hata hivyo, furaha hii inaisha punde wakati Vijay anapoteza nafasi yake katika timu na umaarufu aliokuwa ameupata kwa kuruhusu umaarufu wake umfumbe macho.
Vijay anagundua haraka ni vipi vyombo vya habari na watu wanaweza kumgeuza shujaa kuwa mtu mbaya. Ram hawezi kustahimili madharau na anashikwa na ugonjwa wa ubongo. Nandini anajitolea kumtunza Ram na kumweka Vijay kwake. Vijay na Nandini wanapaa hadi Australia ili afanyiwe upasuaji katika mgongo. Upasuaji unafaulu na Nandini anagundu kuwa rafiki yake wa utoto Nandini anaweza kuwa mwenziwe wa maisha. Anaanza kuwa na hisia za mapenzi kwa Nandini lakini Nandini bado anaendelea kuuguza huzuni ya kugeuziwa mgongo na Vijay na inamwia vigumu kumwamini tena Vijay na kumchukulia kama mwendani wake wa undani ilivyokuwa utotoni. Wanarudi Jaisalmer na Vijay anaapa kubadili mienendo na kuimarisha mchezo wake wa criketi. Alimhakikishia babake na Nandini kuwa anaweza kuichezea nchi yake na Kocha wake anamtegemea pia. Anateuliwa kwa mara nyingine katika kikosi cha kitaifa kucheza katika shindano kuu la kimataifa. Anapata jeraha wakati wa mchezo lakini bado anasisitiza kuendelea na mechi. Anashinda shindano hilo na kurudi nyumbani Jaisalmer, kumwona babake na Nandini. Vijay na babake wanapatana na wakati hali inaelekea kuwa sawa, Ram anaaga dunia katika mikono ya Vijay. Wanatayarisha mazishi na Vijay na Nandini wanaonekana wakifarijiana katika onyesho la mwisho. Tunajiamulia kuwa wanakuja pamoja kama wapenzi. Filamu inaishia Vijay akiichezea timu ya Taifa kwa mara nyingine, akichezea nchi yake, babake na dini yake. .[1][2][3]
Wahusika
haririMwigizaji | Jukumu la Uhusika |
---|---|
Harman Baweja | Vijay Shekhawat |
Amrita Rao | Nandini |
Anupam Kher | Ram Shekhawat |
Gulshan Grover | Andy Singh |
Dalip Tahil | Indian Team Coach |
Uonekanaji wa pekee
haririVictory inawaangazia spesheli wengi wa wachezaji wa sasa na wa awali wa criketi ya kimtaifa kutoka India, Pakistan, Australia, South Africa, Sri Lanka na New Zealand. Hili limefanywa ili kuipa filamu uhalisi na uhai. Baadhi ya wachezaji walioangaziwa ni pamoja na:
- Kamran Akmal
- Mohinder Amarnath
- Rao Iftikhar Anjum
- Allan Border
- Stuart Clark
- Martin Crowe
- Dilhara Fernando
- Brad Haddin
- Brad Hogg
- Mike Hussey
- Sanath Jayasuriya
- Dean Jones
- Simon Jones
- Suresh Raina
- Rohit Sharma
- Dinesh Karthik
- Praveen Kumar
- Brett Lee
- Farveez Maharoof
- Sajid Mahmood
- Shoaib Malik
- Dimitri Mascarenhas
- Ajantha Mendis
- Albie Morkel
- Morne Morkel
- Muttiah Muralitharan
- Ashish Nehra
- Andre Nel
- Yusuf Pathan
- Ramesh Powar
- Kumar Sangakkara
- Ishant Sharma
- Navjot Singh Sidhu
- Harbhajan Singh
- Maninder Singh
- RP Singh
- Michael Slater
- Graeme Smith
- Pat Symcox
- Sohail Tanvir
- Chaminda Vaas
- Atul Wassan
- Waqar Younis
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 "England duo land Bollywood roles". BBC. Iliwekwa mnamo 2008-01-02. Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; name "Victory" defined multiple times with different content - ↑ "Victory news!!". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-02. Iliwekwa mnamo 2010-01-21.
- ↑ "victory movie plot". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-08. Iliwekwa mnamo 2010-01-21.
Viungo vya nje
hariri- IMDb entry
- Official website
- Victory Moving Pictures Archived 17 Januari 2009 at the Wayback Machine.
- Victory at Bollywood Hungama
- Subhash K. Jah film review