Vielezi vya wakati
Mifano |
---|
|
Vielezi vya wakati (alama yake ya kiisimu ni: E) ni maneno yanayofafanua kielezi kwa kujulisha wakati ambao kitenzi hicho kinatendeka/kimetendeka.
Uchambuzi
haririVielezi vya wakati vinaweza kuwa vya:
- Majina ya siku (yaani, Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi, Jumapili)
- Wiki
- Majina ya miezi
- Mwaka
- Majira ya mwaka
- Nyakati za siku
- Matukio ya Kihistoria, n.k.
- Mifano
- Harusi yake itafungwa Jumapili (hapa inataja majina ya siku katika juma).
- Nitasafiri wiki ijayo (hapa inataja wiki)
- Jambazi sugu ameuawa leo usiku (hapa inataja wakati mara mbili, yaani, leo siku ambayo tendo limetendeka halkadhalika muda wa tukio husika ni nyakati za usiku).
- Wakulima hupanda wakati wa vuli (hapa inarejea majira ya mwaka, yaani, vuli, masika, kiangazi, na kipupwe)!
- Ashura alitoroka majogoo (hapa inarejea nyakati za usiku, yaani, majogoo - kuanzia saa tisa usiku hadi kumi na dakika 59).
- Masanja alizaliwa wakati wa vita ya majimaji (hapa inarejea tukio la kihistoria).
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vielezi vya wakati kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |