Vielezi
Mifano |
---|
|
Kielezi (alama yake ya kiisimu ni: E, ing. adverb) ni neno au maneno yanayotoa taarifa ihusuyo kitenzi. Maneno hayo (vielezi) huelezea/hufafanua na kupambanua au kuongeza maana zaidi ya namna au jinsi tendo linavyotendeka - idadi au kiasi cha kutendeka kwa tendo hilo, mahali ambapo tendo linatendeka.
Hivyo basi kielezi ni neno au maneno yanayotoa taarifa ili kukujulisha kuwa kitenzi hicho kimetendeka namna gani au jinsi gani, mara ngapi au kwa kiasi gani, wapi, lini na kwa sababu gani.
Wakati mwingine vielezi hutoa taarifa inayohusu nomino, viwakilishi, vivumishi na hata vielezi vyenzake.
Uchambuzi
Mifano ya jumla
- Mtoto huyu analia sana (mtoto = nomino, huyu = kivumishi, analia = kitenzi kikuu, sana = kielezi cha namna au jinsi ambavyo huyo mtoto kilizi analia).
- Kassim anatembea kitoto (Kassim = nomino, anatembea = kitenzi kikuu, kitoto = kielezi cha namna au jinsi huyo Kassim anavyotembea kitoto).
- Chakula kimepikwa mara mbili (chakula = nomino, kimepikwa = kitenzi kikuu, mara mbili = kielezi cha idadi au kiasi, yaani mara mbili).
- Wanafunzi wamo darasani (wanafunzi = nomino, wamo = kitenzi kishirikishi, darasani = kielezi cha mahali)
- Mvua imenyesha leo mchana (mvua = nomino, imenyesha = kitenzi kikuu, leo = kielezi cha wakati, mchana = kielezi cha wakati
- Steve alikwenda dukani usiku (Steve = nomino, alikwenda = kitenzi kikuu, dukani = kielezi cha mahali, usiku = kielezi cha wakati)
- Mariamu alizaliwa wakati wa ukoloni (Mariamu = nomino, alizaliwa = kitenzi kikuu, wakati wa ukoloni = kitenzi cha wakati
Aina za vielezi
- Vielezi vya namna au jinsi
- Vielezi vya idadi au kiasi
- Vielezi vya mahali au sehemu
- Vielezi vya wakati au muda
Vielezi vya namna au jinsi
Huelezea jinsi au namna jambo linavyotendeka.
Vielezi vya idadi au kiasi
Huelezea kitendo kilifanyika mara ngapi.
Vielezi vya mahali au sehemu
Huelezea kitendo kilifanyika sehemu gani.
Vielezi vya wakati au muda
Huelezea zaidi wakati au muda kitendo kinapofanyika, kwa mfano: jioni, usiku, asubuhi n.k.
Tazama pia
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vielezi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |