Vifaa vya Deni (Soko la Hisa la Nairobi)
Kifaa cha deni ni mkopo. Mwombaji hutoa ahadi ya kulipa riba fulani kila robo au nusu mwaka kuanzia tarehe fulani baada ya kupata mkopo huo na pia uahidi kulipa mkopo uliopewa. Hivyo basi, faida kutoka kwa kifaa cha deni hutokana na riba. Kwa sasa hivi, vifaa kadhaa za deni vina kiwango cha riba cha asilimia 14, 12, 01, 8 kutegemeana na aina ya kifaa hicho na siku kiliyosajiliwa. Katika Soko la Hisa la Nairobi waweza kununua na kuuza vifaa vya deni.
Ni nani anayeweza kuomba fedha
haririNchini Kenya, makampuni na serikali ndiyo yanaweza kuomba fedha kupitia vifaa vya deni katika soko la hisa. Katika masoko mengine ya hisa, hospitali, vyuo vikuu, mashule na vyama vinaweza kuomba fedha kupitia njia hii ikiwa wanaaminiwa na umma.
Kununua kifaa cha deni
haririKatika Soko la Hisa la Nairobi bei ya chini zaidi ya kununua kifaa cha deni ni KShs. 100,000. Unaponunua kifaa cha deni cha kampuni fulani, basi wewe huwa umekopesha kampuni hiyo fedha iliyosambamba na bei ya vifaa vya deni ulivyonunua.
Ni nani anayeweza kununua
haririMtu yeyote wa kibinafsi, Kampuni ya Uwekezaji, Kanisa, Shule, Chuo Kikuu, Kampuni ya Bima na idara nyingine nyingi.
Kuuza kifaa cha deni
haririWakati wa mahitaji ya kighafla, mwekezaji anaweza kuuza vifaa vya deni alivyonunua katika soko kwa urahisi kwani faida ya kifaa cha deni huongezeka kila siku hivyo basi huwa na bei mpya kila siku. Hivyo basi, mwekezaji anaweza kuuza vifaa vyake vya deni siku yoyote kabla ya siku yake ya kukomaa bila kutozwa faini yoyote.
Hata hivyo, panapokuwa na wauzaji wengi katika soko, bei ya vifaa vya deni hushuka na kisha kupanda wanapopungua.
Angalia pia
haririViungo vya nje
hariri- Soko la Hisa la Nairobi Ilihifadhiwa 3 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
- "Capital Markets Authority"
- CDSC Kenya