Vita ya wenyewe kwa wenyewe
Vita vya wenyewe kwa wenyewe ni vita vinayopigwa ndani ya nchi kati ya vikundi vya taifa moja, tofauti na vita vya kimataifa.
Kuna aina nyingi jinsi vita ya wenyewe kwa wenyewe inaweza kutokea:
- kati ya serikali na wapinzani wake wakiamua kutumia silaha
- kati ya vikundi visivyo vya serikali
- kama watu wa sehemu ya nchi wanataka kujitenga na taifa dhidi ya mapenzi ya serikali.
Vita za aina hiyo huwa na ukali, vifo na uharibifu mwingi. Mara nyingi kanuni za vita haziangaliwi na raia wa kawaida huteseka.
Mifano ya nchi zenye vita za wenyewe kwa wenyewe ni:
- Afghanistan (tangu 1978)
- Lybia (tangu 2011)
- Kongo (tena tangu 2007)
- Somalia (tangu 1988/1991)
- Syria (tangu 2013)
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |