Vitenzi vishiriki vipungufu

Mifano
  • Ninyi ndinyi walimu wao
  • Wao ndio mwalimu wao
  • Sisi ndisi walimu wao
  • Huku ndiko alikoenda
  • Hapa ndipo anapoishi

Vitenzi vishirikishi vipungufu (alama yake ya kiisimu ni: t) ni vitenzi chenye mzizi wa NDI-. Vitenzi hivi hujulisha msisitizo wa jambo. Vitenzi vishirikishi vipungufu huchukua viambishi vya nafsi na viambishi vya ngeli vya urejeshi.

Uchambuzi hariri

Kuna mizizi miwili ya vitenzi vishirikishi vipungufu. Navyo ni mzizi wa nafsi na ngeli za urejeshi.

(i) Nafsi hariri

Nafsi Umoja Wingi
I Mimi Sisi
II Wewe Ninyi/nyinyi
III Yeye Wao
Mifano
  • Mimi ndimi mwalimu wao
  • Sisi ndisi walimu wao
  • Wewe ndiwe nwalimu wao
  • Ninyi ndinyi walimu wao
  • Yeye ndiye mwalimu wao
  • Wao ndio mwalimu wao

(ii)Vya ngeli vya urejeshi hariri

Mifano
  • Hizi ndizo ndizi zake
  • Hiki ndicho kitabu chake
  • Hili ndilo shamba lao
  • Humu ndimo alimoingia
  • Hapa ndipo anapoishi
  • Huku ndiko alikoenda

Tazama pia hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vitenzi vishiriki vipungufu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.