Kituo cha umeme
(Elekezwa kutoka Vituo vya umeme)
Kituo cha umeme ni kiwanda ambako umeme unatengenezwa. Kwa kawaida kina idadi ya majenereta yanayotumia teknolojia ya sumakuumeme. Mara nyingi nguvu ya kuzungusha jenereta inapatikana kwa kutumia mvuke wa maji yaani mwendo wa mvuka huzungusha rafadha inayoendesha jenerata.
Mvuke huu hutengenezwa kwa moja ya njia zifuatazo:
- kuchoma fueli kisukuu kama makaa mawe, gesi asilia au petroliamu ili kuchemsha maji
- Tanuri la nyuklia na joto lake linachemsha maji hadi kuwa mvuke
- kutumia Joto kutoka ardhi kwa kuchemsha maji
- kutumia joto la jua kwa mitambo inayokusanya joto hili kuchemsha maji
Vituo vingine vinatumia miendo asilia kama vile
- Umememaji ambako nguvu ya mwendo wa maji kutoka mahali pa juu kutelemka chini inazungusha rafahda za jenereta
- Kutumia nguvu ya upepo vilevile na vituo vyake vimeenea katika miaka ya nyuma kwa uzalishaji umeme
Injini ya mwako ndani inaweza pia kuendesha majenereta.
Katika miaka iliyopita vituo vikubwa vya umemejua vimejengwa na vimekuwa vyanzo muhimu vya umeme katika nchi mbalimbali.