Vivumishi vya kumiliki
Mifano |
---|
*Maneno kama -ake, -ako, -angu, -ao na -etu huitwa pia vivumishi vimilikish. |
Vivumishi vya kumiliki ni maneno yanayotoa taarifa ya kujulisha umiliki wa nomino. Maneno hayo hujulisha kuwa nomino hiyo iliyotajwa ni mali ya nani.
Mchanganuo
haririMashina ya vivumishi vya kumiliki yanajikita katika nafsi:
Nafsi | Umoja | Wingi |
---|---|---|
I | -angu | -etu |
II | -ako | -enu |
III | -ake | -ao |
- Mifano
Nafsi ya kwanza:
- Nyumba yangu imebomoka - umoja
- Shamba langu limelimwa - umoja
- Mtoto wetu amepotea - wingi wake
Nafsi ya pili:
- Nyumba yako imebomoka - umoja
- Shamba lako limelimwa - umoja
- Mtoto wenu amepotea - wingi wake
Nafsi ya tatu:
- Nyumba yake imebomoka - umoja
- Shamba lake limelimwa - umoja
- Mtoto wao amepotea - wingi wake
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vivumishi vya kumiliki kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |