Kiwakilishi nafsi

(Elekezwa kutoka Viwakilishi vya nafsi)
Mifano
  • Mimi, wewe*.
  • yeye, sisi, nyinyi/ninyi, na wao.

*Maneno kama -ake, -ako, -angu, -ao na -etu huitwa viwakilishi/kiwakilishi vimilikishi/kimilikishi.

Kiwakilishi nafsi (pia: Kiwakilishi cha nafsi) ni aina ya neno/maneno yanayosimama badala ya majina yanayotaja nafsi za watu. Viwakilishi vya nafsi hugawanyika katika makundi mawili, nayo ni:

  • Viwakilishi vya nafsi huru
  • Viwakilishi vya nafsi kiambata

Mchanganuo

hariri

Viwakilishi vya nafsi huru

hariri

Haya ni maneno mazima yanayoweza kusimama peke yake bila kuambatanishwa katika neno au mzizi wa neno jingine.

Nafsi Umoja Wingi
I Mimi Sisi
II Wewe Ninyi/nyinyi
III Yeye Wao
Mifano zaidi
  • Mimi ni mwalimu
  • Sisi ni walimu
  • Wewe ni mwalimu
  • Nyinyi ni walimu
  • Yeye ni mwalimu
  • Wao ni walimu

Viwakilishi vya nafsi kiambata

hariri

Hizi ni mofimu tegemezi/vipande vya maneno vinavyoambikwa/vinavyoambatanishwa katika neno au mzizi wa neno jingine ili kudokeza nafsi inayohusika. Mfano: Nikija nitawapeleka, Tukisoma tutafaulu, Ukija utakiona cha moto, Mkija atawaona, Asiyekujua hakuthamini, Waliosafiri wamefika salama.

Nafsi Umoja Wingi Mzizi
I Ni Tu Nikija/Tukija
II U M Ukija/Mkija
III A Wa Akija/Wakija

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  • Massamba, David. 2004. "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiwakilishi nafsi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.