Viwakilishi vya pekee
Mifano |
---|
|
Viwakilishi vya pekee ni viwakilishi ambavyo hubainisha nomino ambayo hutajwa kwa kutumia viambishi vya -ote, -o-ote, -enye, -enyewe, na -ingine. Viwakilishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimoja hutoa taarifa tofauti (ya peke yake) na chenzake. Kimsingi mizizi yake ipo mitano.
Mchangunuo wa mizizi
hariri(i) -ote
haririMaana hasa ni hali ya "kutokubaki na kitu" ukiwa mazungumzoni.
- Mifano
- Yote yamemwagika
- Wote wameondoka
- Zote zimeoza
- Chote kimeliwa
- Sote tutafaulu
(ii) -o-ote
haririMaana hasa ni hali ya kutokuchagua au "pasipo uchaguzi".
- Mifano
- Yeyote aje
- Chochote nitakula
- Lolote nitapanda
- Zozote zitaliwa
- Yoyote inampendeza
(iii) -enye
haririMaana hasa ni hali ya "umiliki". Hudhihirisha dhana ya kuwa na, umilikaji wa mali, tabia, hali na cheo.
- Mifano
- Wenye maji umepasuka
- Mwenye nyumba amehama
- Lenye kutu limetoboka
- Chenye rangi ni changu
- Vyenye sukari nyingi havifai
(iv) -enyewe
haririMaana hasa ni hali ya "msisitizo".
- Mifano
- Mwenyewe amehama
- Lenyewe limetoka
- Yenyewe imebomoka
- Chenyewe kimechomoka
- Kwenyewe kumeanguka
(v) -ingine
haririMaana hasa ni hali ya "nyongeza".
- Mifano
- Mwingine amehama
- Lingine limeliwa
- Nyingine imejengwa
- Kingine kimepotea
- Vingine vimeletwa
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Viwakilishi vya pekee kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |