Volti
(Elekezwa kutoka Volt)
Volti ni kizio cha umeme tuli au kani mwendoumeme ambao ni tofauti ya utuli baina ya mahali pawili kwenye waya kipitishio na huchukua mkondo usiobadilika wa ampea 1 kama nguvu kati ya sehemu pawili ni wati moja.
Kifupi chake ni V.
Fomula yake ni
Maana yake volti moja ni sawa na hisa ya wati 1 gawanya kwa ampea 1.
Volti ni kipimo cha SI. Jina limetolewa kwa heshima ya mwanafizikia Alessandro Volta kutoka Italia.
Ngazi za volti
haririViambishi awali | Desimali |
---|---|
µV 1 (mikrovolti) | V 0,000 001 |
mV 1 (milivolti) | V 0,001 |
V1 (volti) | V 1 |
kV 1 (kilovolti) | V 1 000 |
MV 1 (megavolti) | V 1 000 000 |
GV 1 (gigavolti) | V 1 000 000 000 |