Waamba (kwa lugha yao: Baamba) ni kabila la Kibantu wanaoishi kusini kwa ziwa Albert, upande wa Uganda (Wilaya ya Bundibugyo) na kidogo upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (mkoa wa Kivu Kusini).

Wanakadiriwa kuwa 40,000 hivi.

Lugha ya wengi wao ni Kiamba (Kwamba, pia: Bulebule, Hamba, Humu, Kihumu, Ku-Amba, Kuamba, Lubulebule, Lwamba, Ruwenzori Kibira na Rwamba), mojawapo kati ya lugha za Kibantu.

Tangu zamani ni wakulima, na kwa sasa wengi ni Wakristo[1].

Mwaka 2008 serikali imetambua rasmi Ufalme wa Rwenzururu, ulioundwa na Waamba pamoja na Wakonjo: ndio ufalme wa kwanza wa Uganda unaounganisha makabila mawili.[2]

Tanbihi

hariri
  1. "Amba: A language of Uganda", Ethnologue (accessed 20 August 2009)
  2. "Uganda: Welcome Rwenzururu", editorial by the New Vision, 31 March 2008
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waamba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.