Waangli (kwa Kilatini Anglii, kutoka Angeln, jina la eneo la Ujerumani Kaskazini kwenye bahari ya Baltiki) walikuwa kabila la Wagermanik ambao kutoka huko pamoja na jirani zao Wajuti na baadhi ya Wasaksoni, jumla watu 200,000 hivi, walivamia Britania katika karne ya 5 na baada ya hapo, wakiweka msingi wa Uingereza wa leo.

Ramani ya Dola la Roma na makabila ya Ulaya mwaka 125 BK, ikionyesha makazi ya Waangli kaskazini mwa Ujerumani na kusini mwa Denmark ya leo.
Waangli, Wasaksoni na Wajuti walivyogawana Britania.

Tanbihi hariri

Marejeo hariri