Lambo la Aswan
Lambo la Aswan liko katika Misri ya Kusini kwenye mto Nile. Ukuta wake uko kilomita 13 kusini kwa mji wa Aswan.
Huko maji ya Nile yazuiliwa na kuunda ziwa la Nasser linaloelekea hadi ndani ya Sudani.
Lambo lilijengwa kati ya miaka 1960 - 1970. Shabaha yake kuu ni kuzuia mafuriko ya mto Nile yaliyohatarisha maisha ya watu kando ya mto.
Tatizo kubwa lililojitokeza ni kwamba lilivuruga ekolojia ya mto. Mafuriko yalikuwa yakileta pia matope yenye rutuba yanayobaki sasa ziwani na kujaza polepole ziwa lenyewe. Maji mengi hupotea kila siku kwa njia ya uvukizaji kwa sababu uso kubwa la ziwa uko katika nchi yenye joto kali.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Lambo la Aswan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |