Wakala wa Kimarekani kwa Maendeleo ya Kimataifa

Wakala wa Kimarekani kwa Misaada ya Kimaendeleo ya Kimataifa (USAID) ni wakala huria wa serikali ya Marekani. Wakala hawa ni wahusika wa kwanza kutoa misaada ya raia wa kigeni na maendeleo ya misaada. USAID ni moja ya mawakala wakubwa wa kiserikali wanaotoa misaada duniani, wakiwa na bajeti ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni $27, na pia ni wakala wanaochangia zaidi ya nusu ya misaada ya kimarekani.

Bunge La Marekani lilipitisha sheria “Sharia ya Misaada ya Kigeni” au tarehe nne, mwezi wa tisa, mwaka wa 1961, ambayo ilitambua programu za misaada ya kigeni na kutoa mamlaka ya kuanzisha wakala wa kutoa misaada ya kiuchumi. USAID ilianzishwa kutokana na agizo la kiutendaji la raisi John F. Kennedy, ambaye alihitaji kuunganisha mashirika kadhaa ya misaada ya kiuchumi na programu kuwa chini ya wakala mmoja[1] USAID ikawa shirika la kwanza la misaada ya kigeni ambalo lengo lake la msingi lilikuwa ni maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya muda mrefu.

Mark Green ni Msimamizi wa USAID.

Programu za USAID zimepewa mamlaka na Bunge kwenye Sheria ya Misaada ya Kigeni[2] ambayo Bunge linasaidia kutoa maelekezo ya mwaka ya fedha zinazotolewa kulingana na sharia nyinginezo za Bunge. Kama chombo kimojawapo cha serikali cha sera ya Marekani ya mambo ya nje, USAID inafanyakazi chini ya usimamizi wa Raisi, ofisi ya Katibu Mkuu, na Baraza la Usalma wa Taifa.[3] USAID ina misheni kwenye zaidi ya nchi 100, hasa Afrika, Asia, Amerika ya Kilatini, Mashariki ya Kati, na Mashariki ya Ulaya.

Malengo hariri

Kauli mbiu ya misheni za USAID iliyoanza kutumiwa mnamo Mei 2013 inasema kuwa kuungana ili kutokomeza umasikini wakati huohuo kuimarisha ustahimili, jamii yenye demokrasia na kuboresha usalama, na ustawi wa Marekani.[4]

USAID kupitia mtandao wake kwenye maeneo husika yanayohitaji misaada kutimiza misheni zake, unasimamiwa na serikali ya Marekani kwa programu za nchi zenye kipato cha chini kwa sababu mbalimbali.

Hii inahusisha:

·Msaada kwenye majanga

·Msaada kwenye umasikini

·Ushirikiano wa kiufundi kwenye masuala mbalimbali duniani, ikiwemo mazingira

·Masuala yanayonufaisha nchi nyingine pamoja na Maekani

·Maendeleo ya kijamii na kiuchumi

Msaada kwenye majanga hariri

Baadhi ya programu za misaada ya kigeni ya mwanzoni kutoka kwenye serikali ya Marekani, ilitoa misaada kwenye majanga yaliyotokana na vita. Mwaka 1915, misaada ya USG kupitia kamisheni ya misaada ya Ubelgiji iliyoongonzwa na Herbert Hoover ilizuia njaa kwenye nchi ya Ubelgiji baada ya kuvamiwa na Ujerumani.

USAID inatekeleza juhudi zake za utoaji misaada baada ya vita au majanga ya asili kupitia Ofisi ya Mambo ya Nje ya Marekani ya Misaada ya Majanga iliyopo Washington, D.C. Misaada binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), pamoja na jeshi la Marekani huchangia kwa kiasi kikubwa kutoa misaada kwenye majanga nje ya nchi.

Tanbihi hariri

  1. "USAID History | U.S. Agency for International Development". www.usaid.gov (kwa Kiingereza). 2019-05-07. Iliwekwa mnamo 2019-07-25. 
  2. "Operational Policy (ADS)". www.usaid.gov (kwa Kiingereza). 2017-05-03. Iliwekwa mnamo 2019-07-25. 
  3. "Operational Policy (ADS)". www.usaid.gov (kwa Kiingereza). 2017-05-03. Iliwekwa mnamo 2019-07-25. 
  4. "Mission, Vision and Values | U.S. Agency for International Development". www.usaid.gov (kwa Kiingereza). 2018-02-16. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-02. Iliwekwa mnamo 2019-07-25.