Wakia (kutoka ar. وقية - اوقية awqiyah - waqiyah) ni kati ya vipimo asilia vya Kiswahili ikitaja masi ya takriban gramu 28. Inafanana na kipimo cha kizungu cha aunsi (ing. ounce) inayofafanuliwa kuwa gramu 28.349523125 g. Wakia ya dhahabu (troy ounce) ya Kiingereza hufafanuliwa siku hizi kuwa gramu 31,1034768.

Waswahili wa zamani walipokea kipimo hiki kutoka lugha ya Kiarabu. Katika nchi za Kiislamu wakia ilikuwa sehemu ya 12 ya "ratl" (ratili) lakini ilhali jina la "ratili" iliweza kutaja uzani tofauti sana kati ya gramu 340 hadi kilogramu mbiloi, hata wakia zilitofautiana[1]. Wakia iliyotumiwa katika Afrika ya Mashariki ilifanana na wakia au aunsi asilia ya kale. Matumizi yake ilisanifishwa kwa kutumia sarafu ya reale (yaani sarafu ya Dolar ya Maria Theresa kutoka Austria) kama uzani sanifu.

Tanbihi

  1. Wehr-Cowan wanataja waqiya ya Misri kuwa gramu 37, ya Beirut 213.39, ya Yerusalemu 240, uk 1095

Marejeo

  • Wehr, Hans ed J M.Cowan (1976). A dictionary of modern written Arabic. Wiesbaden - New York: Spoken Language Services Inc. ISBN 0-87950-001-8