Kabila la Lawi
(Elekezwa kutoka Walawi)
Kabila la Lawi (kwa Kiing. Levi) ni mojawapo kati ya makabila ya Israeli ambayo kwa jumla ni 12, kutokana na watoto wa kiume 12 wa Yakobo Israeli. Kabila hilo hutazamwa kama ukoo wa Lawi. Musa alizaliwa katika kabila hilo.[1]
Ndilo kabila la pekee lililoteuliwa na Musa kwa kazi ya ukuhani[2]. Kufuatana na taarifa katika Kitabu cha Kutoka, Musa alifanya azimio hilo baada ya kuona juhudi ya kabila lake wakati wa kuwaondoa wafuasi wa ndama ya dhahabu[3].
Wakati wa kuingia katika nchi ya ahadi, Walawi hawakupokea eneo maalum bali walipewa haki ya kupokea sehemu za sadaka.
Makuhani wa Israeli walikuwa sehemu ya kabila la Lawi. Hadi leo jina la Lawi kwa umbo la Kizungu "Levi" ni jina linalopatikana kati ya Wayahudi.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kabila la Lawi kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |