Wangechi Mutu

Mchongaji wa vinyago wa Kenya

Wangeni Mutu (alizaliwa jijini Nairobi, Kenya, 1972[1]) ni mwanamke msanii wa maonyesho mwenye asili mchanganyiko wa Kenya na Marekani. Anafahamika sana kwa uchoraji, kuchonga sanamu, filamu na kazi zake za maonyesho.[1] Alizaliwa Kenya, aliishi na kuanzisha kazi zake New York kwa zaidi ya miaka ishirini.[1]

Maisha ya awali na Elimu

hariri

Mutu alisoma mwaka 1978 mpaka 1989 Loreta Convent Msongari na baadae United World College of the Atlantic. Alihamia New York miaka ya 1990 huko alibobea katika sanaa ya uchoraji na Anthropolojia katika shule ya The New school kwa ajili ya utafiti wa jamii na Parsons The New School kwa ajili ya ubunifu. Alipata shahada ya uzamili katika uchongaji wa sanamu.[2]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 “Wangechi Mutu Biography”, Gladstone Gallery, Retrieved 24 November 2018.
  2. Posner, Helaine (2013). "Bad Girls: Wangechi Mutu". Katika Heartney, Eleanor (mhr.). The Reckoning: Women Artists of the New Millennium. New York: Prestel. ku. 54–59. ISBN 978-3-7913-4759-2.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wangechi Mutu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.