Wazulu
Wazulu (kwa Kizulu: amaZulu) ni kabila kubwa la Afrika Kusini lenye watu milioni 9-10. Makazi yao ni hasa jimbo la KwaZulu-Natal lakini wako katika miji yote ya Afrika Kusini pamoja na vikundi vidogo zaidi katika Zimbabwe, Zambia na Msumbiji.
Lugha yao ya Kizulu wanayoita wenyewe "isiZulu" ni lugha ya Kibantu.
Katika historia ya Afrika Kusini ufalme wa Wazulu na upanuzi wao chini ya Shaka Zulu ni kipindi muhimu. Dola la Wazulu likatetea uhuru wake hadi 1879 liliposhindwa na Waingereza.
Wakati wa siasa ya apartheid Wazulu kama Waafrika wote walihesabiwa kama raia wa ngazi ya duni.
Tangu mwisho wa apartheid hushiriki kamili katika ujenzi wa taifa.