Wendy Woods
mwalimu wa Africa Kusini na mharakati
Wendy Heather Woods (alizaliwa Bruce; 5 Februari 1941 - 19 Mei 2013) alikuwa mwalimu wa Afrika Kusini na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi.
Woods alifanya kazi na mumewe, mwandishi wa habari Donald Woods, kupinga ubaguzi wa rangi na wote walikimbilia uhamishoni Ufalme wa Muungano mwaka wa 1977. Woods mwenyewe alikuwa mwanachama hai wa Black Sash.
Akiwa uhamishoni, Woods alifanya kazi na mashirika mbalimbali ya misaada na baada ya kifo cha mumewe, alianzisha Wakfu wa Donald Woods. Yeye na familia yake wameshirikishwa katika filamu ya Cry Freedom ya mwaka 1987.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wendy Woods kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |