Werner Forssmann
Werner Forssmann (20 Agosti 1904 – 1 Juni 1979) alikuwa daktari mpasuaji kutoka nchi ya Ujerumani. Pamoja na kazi ya upasuaji alichunguza magonjwa ya moyo na ya mkojo. Alikuwa daktari mpasuaji mkuu katika hospitali za miji ya Dresden na Düsseldorf. Mwaka wa 1956, pamoja na Andre Cournand na Dickinson Richards alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani wa Ulaya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Werner Forssmann kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |