Wesley Moraes

Wesley Moraes (anajulikana kama Wesley; alizaliwa 26 Novemba 1996), ni mchezaji wa soka wa Brazil ambaye anacheza katika klabu ya Aston Villa kwenye Ligi Kuu ya Uingereza na timu ya taifa ya Brazil kama mshambuliaji.

Wesley akiwa Club Brugge.

Timu alizochezeaEdit

TrenčínEdit

Wesley alijiunga na klabu ya AS Trenčín iliyopo Slovak Super Liga mnamo Julai 2015,Mnamo 14 Julai 2015, alichezea Trenčín dhidi ya FCSB katika raundi ya pili ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu wa 2015-2016.

Alifunga goli lake la kwanza akiwa na klabu ya Trenčín kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya FCSB,baada ya timu yake kutoka sare ya 2-2 lakini klabu haikuendelea kwenye raundi inayofuata.[1]

Club BruggeEdit

Wesley alihamia Club Brugge mnamo 29 Januari 2016. Alifunga goli lake la kwanza katika mechi yake ya kwanza dhidi ya KVC Westerlo.

Aston VillaEdit

Mnamo tarehe 13 Juni 2019, Wesley alisaini mkataba katika klabu ya Aston Villa katika Ligi Kuu ya Uingereza, kwa ada ya Pauni 22,000,000.

Wesley alicheza kikosi cha kwanza katika klabu ya Villa kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Minnesota United mnamo 17 Julai 2019.

Wesley alifunga goli lake la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Everton mnamo 23 Agosti, na mgomo wa mara ya kwanza kumpiga Jordan Pickford.

Mnamo tarehe 1 Januari 2020, Wesley alipata jeraha kubwa la maumivu ya goti baada ya kuingiliana na Ben Mee wa Burnley. Wesley alikuwa ameshafunga mapema kwenye mchezo huo,katika mechi ambayo walipata ushindi wa 2-1. Jeraha lake linatabiriwa kuchukua karibu miezi tisa kupona kutoka januari.[2]

TanbihiEdit

  1. https://uk.soccerway.com/matches/2015/07/22/europe/uefa-champions-league/sc-fc-steaua-bucuresti-sa/fk-as-trencin/2049118/
  2. Husband, Ben (2 January 2020). "Details emerge on the severity of Aston Villa striker Wesley's injury". Birmingham Mail. Retrieved 2 January 2020.
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wesley Moraes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.