Wikipedia:Mwongozo (Kurasa za majadiliano)

(Elekezwa kutoka Wikipedia:Majadiliano)
Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    
Fungua hapa na tazama jinsi gani ukurasa wa majadiliano unajazwa katika wikipedia ya Kijerumani!

Kila makala ya wikipedia huwa na "Ukurasa wa Majadiliano". Hii ni sehemu muhimu ya mradi huu na msaada mkubwa wa kuelewana kati ya wanawikipedia na kwa kuboresha makala.

Ukurasa wa majadiliano wa makala

Hapa ni mahali pa kuweka maswali, mapendekezo au maoni juu ya makala - si ndani ya makala!!

Ukurasa wa majadiliano wa watumiaji

Sio kila makala tu hata kila mtumiaji huwa na ukurasa wa majadiliano. Hapa unaweza kuacha ujumbe kwa mtumiaji mwingine.

Kama mtu ameache ujumbe kwenye ukurasa wako utaona sanduku lenye maneno ya kutangaza ujumbe mpya kwako kila ukiingia wikipedia kwa jina lako.

Kuna njia mbili za kujibu ama kwenye ukurasa wako ulipopata swali la mtu mwingine au kwenye ukurasa wake. Ukijibu kwake ataiona akijisajili tena.

Kupanga maandishi yako kwenye kurasa za majadiliano

Unaingia kwa kubofya alama ya "majadiliano" juu ya ukurasa wa uhariri. Usijali kama rangi yake ni nyekundu maana hakuna aliyefungua ukurasa huu na wewe utakuwa mchangiaji wa kwanza.

Ukikuta maandishi tayari weka maandishi yako chini yale yaliyotangulia. Kama unaanzisha mada mapya ni vema kuingiza mstari wa kichwa cha ndani kwa mfano

==Msaada wa makala baobonye==
Salaam nimeona wewe ni mtaalamu wa kompyuta naomba usaidie makala ya baobonye.

Unatakiwa kutia sahihi chini ya jibu lako ama kwa kuandika ~~~~ au kubofya alama katika menyu ya ukurasa wa uhariri.

Si lazima lakini unashauriwa kujiandikisha kwanza kwa jina fulani. Hii haileti gharama kwako lakini utajulikana zaidi inasaidi mawasiliano.

Kujongeza ndani

Ukiingia katika majadiliano na majibu ni vema kutofautisha michango kwa kujongeza ndani. Kawaida ni kujongeza kila jibu hatua moja. Hii inaendelea hatua moja-moja hadi nafasi ya jibu imekuwa nyembamba mno halafu kurudi mbele tena.

Unajongeza maandishi yako ndani kwa kuandika alama ya nukta pacha (:) kwenye nafasi ya kwanza ya mstari na kuandika baadaye. Nukta pacha 2,3,4 zinasukuma maandishi ndani zaidi. Ukianzisha mstari mpya au kuweka alama ya inamaliza kujongeza ndani. Ukitaka kutumia ibara ndani ya mchango wako unahitaji kurudia nukta pacha mwanzoni wa ibara mpya sawa na ibara ya kwanza.

Mfano:

Mstari huu haukujongezwa ndani.
: Nukta pacha inasababisha kujongezwa ndani
:: Mstari huu umejongezwa ndani hatua 2 kwa kutumia nukta pacha 2

itaonekana vile: Mstari huu haukujongezwa ndani.

Nukta pacha inasababisha kujongezwa ndani.
Mstari huu umejongezwa ndani hatua 2 kwa kutumia nukta pacha 2

Alama nene kwa orodha

Ukiandika orodha unaweza kutofautisha mistari kwa alama nene kwa kutumia alama ya kinyota (*) mwanzoni. Kuweka kinyota mara mbili inajongeza mstari ndani pia.

Mfano:

* Mstari wa kwanza
* Mstari wa pili
** Kifungo cha chini cha mstari wa pili
* Mstari wa tatu

itaonekana hivyo:

  • Mstari wa kwanza
  • Mstari wa pili
    • kifungo cha chini ya mstari wa pili
  • Mstari wa tatu

Orodha yenye namba

Orodha yenye namba mfululizo unapata kwa kutumia alama hii: (#). Hata hapa unaweza kutumia alama mbili kwa kuonyesha mistari za ndani.

Mfano:

# Jambo la kwanza
# Jambo la pili
## Nyongeza chini ya jambo la pili
# Jambo la tatu

itaonekana vile:

  1. Jambo la kwanza
  2. Jambo la pili
    1. Nyongeza chini ya jambo la pili
  3. Jambo la tatu