Wikipedia:Makala ya wiki/Mnyamawamtuka

Mnyamawamtuka

Mnyamawamtuka moyowamkia ni aina ya dinosauri ambaye visukuku vyake viligunduliwa kuanzia mwaka 2004 katika bonde la mto Mtuka upande wa kusini ya Ziwa Rukwa, karibu na kata ya Totowe.

Jina la Mnyamawamtuka linarejelea mahali ambako mifupa yake viligunduliwa yaangi bonde la mto Mtuka. Sehemu ya pili ya jina „mkiawamoyo“ imechaguliwa kutokana na umbo la mifupa ya mkia wake inayofanana na umbo la moyo. Mnyamawamtuka m. ni kati ya aina chache za dinosauri zenye majina ya Kiswahili, pamoja na jenasi ya Shingopana.

Mwili wake ulifanana kiasi na mjusi lakini alikuwa kubwa sana, akiwa na na kiwiliwili kikubwa, shingo ndefu, kichwa kidogo na mkia mrefu. Alikula majani. Mnyama aliyepatikana kweye mto Mtuka alikuwa kijana bado ambayo hakufikia vipimo vya mkubwa. Alikuwa na takriban tani 1.5, alikuwa na urefu wa mita 1.5 kiunoni akiwa na urefu wa mita 7.6 kuanzia kichwani hadi mwisho wa mkia wake. ►Soma zaidi