Wikipedia:Mwongozo

(Elekezwa kutoka Wikipedia:Ukufunzi)
Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    

Mwongozo wa kuhariri Wikipedia – Utangulizi

Wikipedia ni kamusi elezo katika intaneti inayojengwa na jumuiya ya washiriki nawe unaweza kuchangia. Mwongozo huu utakusaidia kuwa mchangiaji wa Wikipedia.

Kurasa zifuatazo zitakupa mwongozo kuhusu mtindo na makala za Wikipedia zilivyo, na kukuelezea kuhusu jumuia ya Wikipedia na sera muhimu za Wikipedia na makubaliano.

Huu ni mwongozo wa kimsingi tu, na siyo maelekezo ya kirefu. Iwapo unataka maelezo zaidi, kuna viungo kuelekea kurasa nyingine kwa maelezo zaidi. Kuzisoma na kuzielewa, unaweza ukazifungua katika kivinjari tofauti au katika dirisha la tabo.

Kuna viungo kuelekea katika kurasa za "sanduku la mchanga" ambapo unaweza kujipatia uzoefu kile unachojifunza. Hebu jaribu vitu tofauti na uchezecheze! Hakuna mtu atakayechukizwa endapo utavuruga na jaribio katika maeneo ya vitendo.

Ilani: Mwongozo umetoa maelezo yanayofaa hasa kwa wale wanaotumia umbo la kurasa la MonoBook. Tangu Septemba 2010 umbo la kurasa kama inavyoonekana kwa watumizi wasioingia akaunti ni Vector. Mwongozo bado haujaandikwa upya. Wale walioingia akaunti zao wanaweza kubadilisha umbo la kurasa kwenye mapendekezo yao. Umbo nyingine zinaweka viungo mahali tofauti kwenye ukurasa, na kama ni hivyo maelezo ya kupata viungo hayataeleweka moja kwa moja.