Wimbo kwa Afrika
Song for Africa (SFA) ilikuwa shirika lisilo la faida nchini Kanada lililoanzishwa mnamo 2006 na mtayarishaji wa muziki na sinema Darcy Ataman. Washiriki wa programu ya Song for Africa walijifunza jinsi ya kuandika, kutekeleza na kusambaza muziki wao kupitia vituo vya redio katika maeneo yao. Song for Africa ilifanya kazi nchini Kenya, Rwanda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Historia
haririMwaka 2006 wanamuziki kadhaa wa Kanada waliungana kuandika na kurekodi wimbo "Song for Africa" kwa shabaha ya kuongeza uelewa wa janga la UKIMWI barani Afrika. Baada ya kuonyeshwa kwa wimbo huo kweneye Mkutano wa Kimataifa wa UKIMWI huko Toronto, shirika la 'Song for Africa' (SFA) liliibuka kama njia ya wasanii wanaoshiriki kukuza zaidi juhudi katika mapambano dhidi ya VVU / UKIMWI.
Kwa kushirikiana na shirika la Free The Children na CARE Kenya, filamu ilitolewa na 'Song for Africa' iliyosimulia hadithi za kila siku za jamii zilizoathiriwa na VVU / UKIMWI. Ian D'Sa (Billy Talent), Damhnait Doyle, Luka McMaster na Simoncox walishiriki katika filamu hiyo.
FIliamu iliyofuata mwaka 2009 ilikuwa Rwanda: Rises Up![1] iliyolenga kuonyesha nguvu ya taifa la Rwanda jinsi ilivyopoa baada ya mauaji ya kimbari ya 1994. Albamu ya kuambatana na filkamu ilitolewa na Sony Music ikaonyesha wasanii wa Kanada wakiwemo Sarah Slean, Steve Bays (Hot Hot Heat), Damhnait Doyle na Tim Edward (Crash Parallel) walioshiriki kwenye filamu, na pia Ian D'Sa (Billy Talent) , Cone McCaslin (Sum 41 / Operesheni MD), Classified, na The Trew.
Kwa sasa (2021) hakuna habari kazi ya Song for Africa ilikwisha rasmi lini; ila Darcy Ataman ameendelea kusafiri kwenda Rwanda, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kujenga kampuni ya Make Music Matter inayoendesha miradi ya kutumia muziki [2] kama tiba kwa watu walioathiriwa na vurugu kali, kama vita, mauaji ya kimbari au kwa wanawake waliowahi kubakwa.
Filamu
haririAlbamu
hariri- Song for Africa [5]
- Rwanda: Rises Up!
Marejeo
hariri- ↑ "Darcy Ataman". Samaritan Mag (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-08-17.
- ↑ https://www.huffpost.com/author/darcy-ataman
- ↑ Song for Africa Documentary (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2021-08-17
- ↑ Rwanda: Rises Up! Trailer (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2021-08-17
- ↑ Rwanda: Rises Up! Trailer (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2021-08-17