Wingu vundevunde
Wingu vundevunde (kwa Kilatini/Kiingereza: cirrus, "shungi la nywele") ni wingu la fuwele za barafu linalopatikana kwa kimo kikubwa. Mawingu vundevunde huonekana kama nyuzi nyeupe au kanda nyembamba angani[1].
Mawingu hayo hutokea kwenye kimo cha mita 16,500 hadi 45,000.
Kutoka kwenye uso wa Dunia, mawingu vundevunde huonekana kuwa na rangi nyeupe au kijivu. Yanaundwa wakati mvuke wa maji hupitia kimo cha mita 5,500 ambako baridi huongezeka, hivyo mvuke unaganda na kuunda fuwele za barafu.
Kwa kawaida kimo cha mawingu hayo ni mita 8,000–12,000 juu ya usawa wa bahari.
Tanbihi
hariri- ↑ Funk, Ted. "Cloud Classifications and Characteristics" (PDF). The Science Corner. National Oceanic and Atmospheric Administration. Iliwekwa mnamo 30 Januari 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya Nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- A cloud atlas with many photos and description of the different cloud genera Ilihifadhiwa 31 Julai 2020 kwenye Wayback Machine.
- UIUC.edu's online guide to meteorology Ilihifadhiwa 15 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.
- International Cloud Atlas – Cirrus Ilihifadhiwa 17 Machi 2014 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wingu vundevunde kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |