World Literacy Foundation

World Literacy Foundation (kifupi: WLF) ni jina la kutaja asasi ya kiraia isiyolenga faida kwa ajili ya kuwainua vijana katika ujuzi na maarifa ya kujua kusoma na kuandika.

Watoto wakiwa wamebeba nembo ya WLF Arusha Tanzania

Taasisi hiyo ilianzishwa nchini Australia mwaka 2003, ikisimama katika misingi ya haki ya elimu pamoja na kutangaza umuhimu wa elimu katika jamii.

Taasisi hiyo imekuwa ikihusisha jamii katika kujengea uelewa juu ya umuhimu wa elimu pamoja na kuwa na mabalozi katika nchi mbalimbali duniani, na inaarifiwa kuwa kila mwaka mmoja kati ya watu kumi, hajui kusoma na kuandika huku watu milioni 750 dunia kote hawajui kusoma na kuandika.[1]

Marejeo hariri

  1. "Literacy". UNESCO (kwa Kiingereza). 2013-04-25. Iliwekwa mnamo 2019-05-07. 
  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu World Literacy Foundation kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.