Balozi ni mwakilishi rasmi wa serikali ya nchi yake katika nchi nyingine. Anatumwa huko na wizara ya mambo ya nje akitazamiwa kama mwakilishi wa mkuu wa nchi inayomtuma.

Balozi Chokala kutoka Tanzania akikabidhi barua rasmi ya kutambulishwa kwa rais wa Urusi Vladimir Putin.

Kwa kawaida anaongoza ofisi ya ubalozi ambako anasaidiwa na maafisa wengine wanaotumwa katika utaratibu wa diplomasia.

Nchi zinazopokea ubalozi zinakubali pia huria ya kidiplomasia inayomaanisha ya kwamba balozi na wanadiplomasia wenzake hawawezi kukamatwa wala kuadhibiwa katika nchi wanapotumwa kwa kosa lolote. Vilevile majengo ya ubalozi hutazamwa kama ardhi ya nchi nyingine ambako polisi ya nchi ulipo haiwezi kuingia. Mzigo wake haiwezi kufunguliwa na maafisa wa forodha au polisi katika nchi alikotumwa. Utaratibu huu ulikubaliwa katika Mkataba wa Kimataifa wa Vienna kuhusu Diplomasia.

Balozi mpya anatumwa na barua rasmi kutoka wizara yake akikubaliwa na nchi anapohudumia. Nchi inayompokea inaweza kumwambia pia aondoke tena.

Balozi hutumwa kwenda nchi nyingine kwa miaka kadhaa akirudi baadaye katika nchi yake ambako anaweza kuendelea kufanya kazi ndani ya wizara au kutumwa tena kwa nchi nyingine.

Matumizi mengineEdit

Nchini Tanzania jina "balozi" hutumiwa pia kumtaja "balozi wa nyumba kumi" (kwa Kiingereza ten cell leader) ambaye ni mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi katika eneo la nyumba kumi za jirani.[1]

  1. Kevin Croke, Strategies of Single Party Hegemony in Tanzania , taarifa juu ya utafiti ulioendeshwa na Benki ya Dunia mnamo , Journal Democratization Volume 24, 2017 - Issue 2zania: Evidence from Survey Experiments