Yohane IV
Yohana IV (jina la awali: Dejazmach Kassay; 1831 - Metemma, Sudan, 10 Machi 1889) alikuwa Ras wa Tigray na Kaisari wa Ethiopia kati ya miaka 1872–1889.
Baada ya kumshinda Tekle Giyorgis II vitani, alimfuata Tewodros II katika kutawala juu ya majimbo yote ya Ethiopia.
1876 aliweza kuzuia mashambulio ya Misri dhidi ya Ethiopia.
Aliuawa katika mapigano ya Metemna dhidi ya jeshi la Mahdi tarehe 10 Machi 1889. Kichwa chake kilikatwa na kuonyeshwa baadaye mjini Omdurman.
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Uhabeshi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yohane IV kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |