Young Killer Msodoki


Eric Msodoki maarufu kama Young Killer Msodoki , ni rapa na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania ambaye alipata umaarufu mkubwa mwaka 2013 baada ya kuachia wimbo wake wa kwanza wa "Dear Gambe". Wimbo huo aliomshirikisha msanii Bele9. Hatua hiyo ilifungua milango na fursa nyingi, na kupelekea yeye kushinda tuzo ya Msanii Bora Aliechipukia kutoka Tanzania.[1]

Tangia wakati huo msanii huyo mzaliwa wa Mwanza amekuwa akibariki mashabiki kwa vibao vyake mfululizo kama New Girlfriend Story, Secreto, Sinaga Swagger, Exclusive Interview, Rudia, Toto Tundu na nyimbo zingine nyingi ambazo zilipokelewa vyema na mashabiki wa muziki wa bongo fleva. Tangu kuwanza harakati zake za kimziki hadi sasa Young Killer ana Albums tatu alizo toa mwaka 203 ,2022 na 2024. Msanii huyo ametajwa kuwa miongoni mwa watunzi bora wa nyimbo katika historia ya Hip-hop ya Tanzania.

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Young Killer Msodoki kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.