"Zilipendwa" ni jina la wimbo uliotoka 25 Agosti, 2017 wa kundi zima la muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - WCB. Wimbo umetayarishwa na Laizer Classic. Huu ni wimbo wa kwanza kutolewa kama kikosi kizima cha WCB tangu kuanzishwa kwake. Vilevile wiambo unamtambulisha Malomboso wa Yamoto Band kuwa mwanachama kamili wa WCB tangu kuvunjika kwa Yamoto Band. Wimbo umetolewa masaa 12 tangu kutolewa wimbo wa Ali Kiba Seduce Me. Wimbo ulikuwa gumzo sana wakati umetoka hasa kwa kufuatia malumbano yaliyoendelea mtandaoni huku kukiwa na hisia kadhaa wa kadhaa ya kwamba kautoa wimbo huu ni jibu la Seduce Me ili kupunguza makali. Wimbo unahusu mambo kadhaa yaliyopita, watu, wanamuziki, watu mashuhuri, na vitu ambavyo vilipendwa na watu wengi hapo awali. Siku moja tu, tangu kutolewa, Matonya 2 akatoa lawama ya kwamba WCB wameiba wazo lake la wimbo ambao aliutoa yeye tarehe 5 Novemba, 2012. Matonya alitoa lake la moyoni kwamba wimbo mzima ni wazo lake na si WCB.[1][2] Vilevile kulikuwa na ushindani mkali sana wa kutazamwa sana katika idhaa ya YouTube. Wimbo ulikuwa unapishana kati ya watazamaji 500,000 hadi 800,000 huku Seduce Me ikiwa juu ya Zilipendwa. Hatimaye zikaja kupishana kiasi tu.

“Zilipendwa”
“Zilipendwa” cover
Kava la Zilipendwa
Single ya WCB
Imetolewa 25 Agosti, 2017
Muundo Upakuzi mtandaoni
Imerekodiwa 2017
Aina Bongo Flava, muziki wa dansi
Urefu 5:25
Studio Wasafi Records
Mtayarishaji Laizer Classic

Tarehe 7 Novemba, 2017, bendi ya muziki wa dansi nchini Tanzania maarufu kama Msondo Ngoma Baba ya muziki wafungua mashtaka ya madai kwa WCB kutumia sehemu ya saxafoni la wimbo wa Ajali katika wimbo huu mwishoni bila ruhusa kutoka kwa wamiliki halali wa melodi ile. Msondo wanataka walipwe pesa za Kitanzania milioni 300 kutoka kwa WCB. Msondo wametoa barua hiyo kupitia wanasheria wao Maxim Advocates kwenda kwa WCB huku nakala kwenda Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) pamoja na COSOTA. Hadi sasa hakuna mrejesho kutoka kwa WCB.[3][4] Habari hii imechukuliwa kwa aina yake katika tasnia ya muziki Tanzania. Wapo waliona ni sawa kudadi haki yao hao Msondo. Wapo waliona hii ni kuendekea njaa na sifa tu katika muziki.[5]

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Zilipendwa ya Matonya katika YouTube
  2. Matonya alalamikia kunakiliwa wimbo wake bila ruhusa MATONYA AELEZA KWANINI ANASEMA NGOMA YAKE IMEIBIWA NA WCB ..NGOMA YA ZILIPENDWA
  3. "Bendi ya Msondo Ngoma Yadai Ilipwe Milioni 300 na WCB Kisa Zilipendwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-13. Iliwekwa mnamo 2017-11-11.
  4. Msondo Ngoma waenda kwa Wanasheria, wanataka WCB wawalipe Milioni 300
  5. Bendi ya Msondo Ngoma yataka ilipwe na WCB milioni 300 kisa Zilipendwa

Viungo vya Nje

hariri