Ziria Tibalwa Waako

Mhandisi wa umeme Uganda na mtendaji mkuu wa shirika la mamlaka ya udhibiti umeme

Ziria Tibalwa Waako ni mhandisi wa umeme wa Uganda na mtendaji mkuu wa shirika, anahudumu kama Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mkuu Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Umeme, kutoka Novemba 2016. Alichukua nafasi ya Benon Mutambi, ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uganda . [1] Kwa miezi minne ya kwanza, kuanzia Novemba 2016 hadi Machi 2017, alihudumu kama kaimu, hadi kuthibitishwa kwake tarehe 27 Machi 2017.

Ana stashahada ya uhandisi wa umeme na Astashahada ya juu ya uhandisi wa umeme, zote alizopata kutoka Uganda Polytechnic Kyambogo (leo Chuo Kikuu cha Kyambogo ). Pia ana Shahada ya Kwanza ya Sayansi na Shahada ya Uzamili ya Sayansi, katika uhandisi wa Umeme, na zote mbili alizipata kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, huko Kampala, mji mkuu wa Uganda na jiji kubwa zaidi. Pia, ana Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara katika Uongozi, iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Walden, huko Minneapolis, Minnesota, Marekani. [2]

Kazi hariri

Kazi ya Tibalwa Waako ni ndefu, inarudi nyuma kwa zaidi ya miaka 23. Maisha yake yote ya kazi ya yametumika katika sekta ya umeme nchini Uganda. Alifanya kazi na Bodi ya Umeme ya Uganda (UEB) ambayo sasa imekufa. UEB ilipovunjwa mwaka wa 2001, alihamishiwa kwa Kampuni ya Usambazaji Umeme ya Uganda (UETCL). Mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa udhibiti wa kiufundi katika Mamlaka ya Udhibiti wa Umeme, akihudumu katika wadhifa huo hadi alipopandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi Mtendaji na wakala wa udhibiti.

Familia hariri

Mhandisi Waako ameolewa na Profesa Paul Waako, mtaalam wa dawa za kimatibabu na msimamizi wa taaluma, ambaye tangu tarehe 1 Mei 2019, anahudumu kama Makamu Chansela wa Chuo Kikuu cha Busitema, chuo kikuu cha umma Mkoa wa Mashariki mwa Uganda. Kwa pamoja ni wazazi wa watoto watano. [3]

Mambo mengine ya kuzingatia hariri

Mhandisi Ziria Tibalwa Waako ni mwanachama wa "Taasisi ya Wahandisi Wataalam wa Uganda".

Marejeo hariri

  1. UBN (30 November 2016). "Electricity Regulatory Authority gets acting chief executive". Uganda Business News (UBN). Iliwekwa mnamo 23 September 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. Jackie Nalubwama and David Lumu (14 June 2020). "Ziria Waako: CEO with a vision for women". New Vision. Iliwekwa mnamo 1 October 2021.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. Busitema University (June 2019). "Profile of Professor Paul Waako: Vice Chancellor Busitema University". Busitema University. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-19. Iliwekwa mnamo 4 November 2019.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)

Viungo vya nje hariri