Ziwa Ziway
Ziwa Ziway au Zway ni kati ya maziwa ya maji baridi ya Bonde la Ufa nchini Ethiopia. Liko kilometa 160 kusini kwa Addis Ababa[1], mita 1,636 [2][3] au 1,846[4] juu ya UB.
Ziwa Ziway | |
---|---|
Anwani ya kijiografia | 8°00′N 38°50′E / 8.000°N 38.833°E |
Nchi za beseni | Ethiopia |
Urefu | km 31 (mi 19) |
Upana | km 20 (mi 12) |
Eneo la maji | km2 440 (sq mi 170) |
Kina kikubwa | m 8.9 (ft 29) |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB | m 1 636 (ft 5 367) |
Visiwa | 5 (Debre Sina, Galila, Bird Island, Tulu Gudo) |
Miji mikubwa ufukoni | Ziway |
Ziwa linachangiwa na Mto Meki na Mto Katar, halafu linatokwa na mto Bulbar[5].
Eneo lake lote ni kilometa mraba 440, urefu ni kilometa 31 na upana kilometa 20. Kina chake hakizidi mita 9.
Mji wa Ziway uko pwani upande wa magharibi.
Ndani yake vinapatikana visiwa vya Debre Sina, Galila, Bird Island na Tulu Gudo, ambacho kina monasteri
Tanbihi
hariri- ↑ Leslau, Wolf (1999). Zway Ethiopic Documents: Grammar and Dictionary. Wiesbaden: Otto Harrassowitz. uk. xv. ISBN 3447041625.
- ↑ "Water Resources and Irrigation Development in Ethiopia – IWMI" Archived 18 Julai 2011 at the Wayback Machine, Table 3. Basic hydrological data of lakes and reservoirs of Ethiopia. (accessed 2 July 2011)
- ↑ Google Earth
- ↑ "Climate, 2008 National Statistics (Abstract)" Archived 13 Novemba 2010 at the Wayback Machine, Table A.2. Central Statistical Agency website (accessed 26 December 2009)
- ↑ Robert Mepham, R. H. Hughes, and J. S. Hughes, A directory of African wetlands, (Cambridge: IUCN, UNEP and WCMC, 1992), p. 158
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Ethiopia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ziwa Ziway kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |