Zukiswa Wanner
Mwandishi wa Afrika Kusini
Zukiswa Wanner (alizaliwa 1976, zambia) ni mwandishi wa riwaya na mhariri huko Afrika Kusini. Zukiswa amezaliwa nchini Zambia na anaishi Kenya. Mnamo mwaka 2006, alipochapisha kitabu chake cha kwanza, riwaya zake ziliorodheshwa kwenye tuzo ikiwa ni pamoja na Tuzo za Fasihi nchini Afrika Kusini (SALA) na Tuzo ya Waandishi wa Jumuiya ya Madola. Mnamo mwaka 2015, alishinda tuzo K Sello Duiker Memorial Literary Award , London, Cape Town Joburg mwaka (2014).[1]
Zukiswa Wanner | |
---|---|
| |
Alizaliwa | 1976 |
Nchi | Zambia |
Kazi yake | mwandishi, mhariri |
Mwaka 2014 alitajwa katika orodha ya Afrika39 ya waandishi 39 wa Afrika chini ya umri wa miaka 40 wenye uwezo wa kufafanua mwenendo katika fasihi ya Afrika.[2]Mwaka 2020 alikuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kushinda tuzo ya Goethe.[3]
Marejeo
hariri- ↑ "2015 South African Literary Awards (SALAs) Winners Announced", Books Live, Sunday Times, 9 November 2015.
- ↑ Africa39 list of artists, Hay Festival.
- ↑ "First African Woman to Be Awarded the Goethe Medal: Zukiswa Wanner". Literandra (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2020-04-28. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-14. Iliwekwa mnamo 2020-04-29.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zukiswa Wanner kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |