Zuzana Čaputová

Mwanasheria wa Kislovakia, mwanaharakati wa mazingira na mwanasiasa

Zuzana Čaputová (alizaliwa 21 Juni 1973) ni mwanasiasa, wakili na mwanaharakati wa mazingira kutoka Slovakia. Ni rais wa tano wa Slovakia, nafasi ambayo ameshikilia tangu 15 Juni 2019. Čaputová ndiye mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa wa urais, vilevile rais mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Slovakia, aliyechaguliwa akiwa na umri wa miaka 45.[1]

Zuzana Čaputová, 2021.

Čaputová alijulikana kwa mara ya kwanza kwa kushinda katika mapambano ya muongo mzima dhidi ya dampo lenye sumu katika mji wake wa Pezinok. Kwa hili, Čaputová alipewa Tuzo ya Mazingira ya Goldman mwaka 2016. Alishinda uchaguzi wa urais wa Slovakia wa 2019 kwa 58% ya kura katika duru ya pili.

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zuzana Čaputová kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.