Shambulio la 11 Septemba 2001

(Elekezwa kutoka 11 Septemba 2001)

Shambulio la 11 Septemba 2001 ni tarehe na mwaka uliotokea mashambulio manne ya pamoja yaliyofanywa na kikosi cha Kigaidi cha al-Qaida dhidi ya Marekani. Kwa mujibu wa taarifa za maofisa, yasemekana kwamba kikosi cha Al-Qaida waliziteka nyala ndege nne wakazitumia kama silaha wakigongesha ndege katika majengo mjini New York na Washington DC kwa makusudi. Karibuni watu 3,000 walipoteza maisha katika shambulio hilo.

Ndege zilitumika kufanyia Ughaini huo

 
Mabaki ya Jengo la WTC.

1. American Airlines Flight 11, iliyotumiwa kugonga mnara wa Kaskazini mwa Jengo la Biashara la Kimataifa (World Trade Center) la mjini New York mnamo saa 8:46:30 asubuhi.

2. United Airlines Flight 175, ilitumiwa kugonga mnara wa Jengo la Biashara la Kimataifa (World Trade Center) la Kusini mnamo saa 9:02:59 asubuhi. Watu wengi waliona tukio la pili kwasababu habari zilikuwa tayari zishasambaa katika mji na kila kamera za televisheni zilikuwa zikielekezea macho yao huko katika eneo la tukio, na wakati huo huo ndege ya pili ikagonga tena mnara wa Kusini mwa Jengo hilo.

3. American Airlines Flight 77, ilitumiwa kugonga jengo la Pentagon la mjini Arlington, Virginia (karibu kidogo na Washington DC), mnamo saa 9:37:46 asubuhi.

4. United Airlines Flight 93, hii haikubahatika kugonga mahala popote pale, badala yake wakaiangusha chini mnamo saa 10:03:11 asubuhi. Yaaminika ya kwamba magaidi hao walikuwa wakitaka kuigonga ndege hiyo katika jengo la mji mkuu wa Marekani. Abiria walijaribu kuinyang'anya Ndege hiyo kutoka mikononi mwa magaidi hao lakini hawakufanikiwa. Na matokeo Ndege ikashia kuanguka karibu na mji wa Shanksville, Pennsylvania.

Matokeo ya maafa hayo

Jumla ya abiria 246 na magaidi 19[1] waliokuwa wasafiri katika dege zote 4 waliuawa wakati wa shambulizi hizo (dege American Airlines 11 - abiria 87[2] na magaidi 5, United Airlines 175 - abiria 60 na magaidi 5[3], American Airlines 77- abiria 59 na magaidi 5, na dege United Airlines 93- abiria 40 na magaidi 4). Minara yote miwili ya jengo la World Trade Center yalipamba moto baada ya shambulio. Mnara wa Kusini (yaani WTC 2) liliungua kwa muda wa dakika 56 kabla ya kuanguka na kuangamia kabisa.

Jengo la Kaskazini (WTC 1) liliungua kwa muda wa dakikar 102 nalo pia lilianguka. Kama jengo la WTC lilivyoanguka, sehemu na mmong'onyoko wa jengo hilo lilipelekea majengo mengine yaliyoyazunguka majengo hayo kushika moto na kuharibika pia. Kutokaa na uharibifu uliotokea, jengo la tatu la 7 World Trade Center (7 WTC), nalo likaanguka mnamo saa 5:20 jioni. Baadahi ya mamjengo mengine yaliharibiwa vibaya na hata kuangamia kabisa yaani.

Takriban watu watu 2,602 walipoteza maisha katika Jengo la World Trade Center.

Ndege iliyogonga Pentagon iligonga chini mwa upande wa Magharibi mwa jengo hilo. Kisha ikagonga mpaka katika nguzo tano zinazoshikiria jengo hilo la Pentagon. Shambulio hilo Pentagon liliuwa watu 125.

Takriban watu 2,973 walikufa katika shambulio hilo, wakiwemo wazima moto 343, wanapolisi wa New York 23, na wanapolisi wa mamlaka ya bandari 37 waliokuwa wakijaribu kuokoa maisha ya baadhi ya watu waliopatwa na balaa hilo.

Hili ndilo shambulio kubwa la kwanza kwa watu wasio Waamerika kushambulia nchini humo tangu mnamo mwaka wa 1941, pale Wajapani waliposhambulia kituo cha jeshi la maji kilichopo katika Bandari ya Pearl, Hawaii. Dhana nyingi zilikuwa zikionekana kwamba kuna watu Marekani waliojua kwamba kutatokea tukio kama hilo kabla na siku liatatendeka.

Vita dhidi ya ugaidi

Baada ya shambulio, Wamarekani wakawa wanawalaumu Al-Qaeda kwa kitendo walicho kifanya. Tangu hapo wakaianza vita dhidi ya Ugaidi. Kiongozi wa al-Qaeda, Osama bin Laden, Alikimbilia nchini Afghanistan. Serikali ya Marekani iliwaambia Serikali ya Afghanistan iliyokuwa mkononi mwa kundi la Kiislamu wa Taliban, kumsalimisha bin Laden mikononi mwao. Wataliban hawakufanya hivyo. Kiongozi wa Wataliban, Mullah Muhammad Omar, aliitaka Serikali ya Marekani impe Uthibitisho unaonyesha kwamba Osama anahusika na tukio hilo. Rais wa Marekani bwana George W. Bush akasema kwamba hakuna haja kutaka Uthibitisho wowote ule na Serikali ya Marekani ikaanzisha vita dhidi ya Afghanistan.

Tanbihi

  1. "National Commission on Terrorist Attacks Upon the United States". govinfo.library.unt.edu. Iliwekwa mnamo 2019-06-25.
  2. "CNN.com - September 11 Memorial". edition.cnn.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-27. Iliwekwa mnamo 2019-06-25.
  3. "CNN.com - September 11 Memorial". edition.cnn.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-27. Iliwekwa mnamo 2019-06-25.

Marejeo

  1. http://www.guardian.co.uk/waronterror/story/0,1361,573975,00.html

Viungo vya nje

  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shambulio la 11 Septemba 2001 kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.