Washington, D.C.
Washington, D.C., rasmi inajulikana kama Wilaya ya Columbia na kwa kawaida huitwa Washington au D.C., ni mji mkuu na wilaya ya shirikisho ya Marekani. Jiji hili liko kwenye Mto Potomac, mkabala na Virginia, na linapakana na Maryland upande wa kaskazini na mashariki. Lilipewa jina la George Washington, rais wa kwanza wa Marekani. Wilaya hiyo imepewa jina la Columbia, mfano wa kike wa taifa.

Jiji la Washington | |||
| |||
Mahali pa mji wa Washington katika Marekani |
|||
Majiranukta: 38°54′36″N 77°0′36″W / 38.91000°N 77.01000°W | |||
Nchi | Marekani | ||
---|---|---|---|
Tovuti: http://www.dc.gov/ |

Jina la mji mkuu limechaguliwa kwa heshima ya kiongozi wa uhuru na rais wa kwanza George Washington. Jina la "District of Colombia" likachaguliwa kwa heshima ya Kristoforo Kolumbus mpelelezi wa Amerika.
Mji wa Washington uko kando la mto Potomac kati ya majimbo ya Maryland na Virginia. Uko karibu na pwani la mashariki la Marekani. Hori ya Chesapeake ya Atlantiki iko 35 km kutoka mji. Anwani ya kijiografia ni 38°53'42"N na 77°2'12"W.
Washington D.C. ni tofauti na jimbo la Washington lililopo upande wa magahribi wa Marekani.
Hapa ni makao rasmi ya Bunge la Marekani, ya Rais pamoja na serikali yake na makao ya mahakama kuu. Kuna pia majengo ya kihistoria hata kama Marekani haina historia ndefu pamoja na makumbusho mazuri.
Historia
haririMakao ya kwanza ya serikali ya Marekani ilikuwa New York. Rais George Washington mwenyewe alichagua eneo la mji mpya kando la mto Potomac mwaka 1790. Ujenzi wa ikulu la Nyumba Nyeupe ulianza 1792. Mpango wa mji ulifuata mfano wa mji wa Karlsruhe (Ujerumani).
11. Juni 1800 Washington ikawa mji mkuu wa Marekani. Wakati wa vita ya Uingereza na Marekani ya 1814 mji ulivamiwa na kuchomwa na Waingereza.
Hadi vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani Washington ilikuwa mji mdogo usiozidi wakazi 75,000 lakini ilikua baada ya vita kwa sababu serikali iliongezeka idara na wafanyakazi.
Tangu 1878 mji wa Washington na mkoa wa shirikisho ("D.C.") viliunganishwa. Mji kama mkoa ulitawaliwa moja kwa moja na bunge. Tangu 1973 mji umempata meya na serikali ya kimanisipaa. Kwenye bunge lenyewe hakuna mbunge wa wakazi wa Washington. Kuna mwakilishi wao mle lakini hana kura.
Viungo vya nje
hariri
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Washington, D.C. kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |